KADHI WA MKOA WA MBEYA ATEMBELEA MSIKITI MPYA UNAOJENGWA MSWISWI

Xmation Media
By -
0

 

Mbeya – Kadhi wa Mkoa wa Mbeya, Sheikh Dkt. Hassan Mbarazi, leo ametembelea msikiti mkubwa unaoendelea kujengwa katika Kijiji cha Azimio, Uswahilini, Kata ya Mswiswi.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mbarazi alipata pia nafasi ya kuiona madrasa iliyoasisiwa na marehemu Sheikh Rashid Mbisa, aliyekuwa Sheikh wa kwanza wa Mkoa wa Mbeya. Madrasa hiyo ni alama ya urithi wa elimu ya dini aliouacha kiongozi huyo kwa jamii.

Ombi la Familia kwa Kadhi

Familia ya marehemu Sheikh Rashid iliomba Kadhi awasaidie kutafuta wafadhili ili msikiti huo ukamilike. Kadhi alipokea jukumu hilo kwa moyo mkunjufu, na aliahidi kulifikisha kwa waumini wa Mbeya na maeneo mengine anayoyafikia, Inshallah.

Waliokuwepo

Katika safari hiyo, Kadhi aliongozana na Imam Ilyasa Nchalikwao, Imam wa Masjid Tawfiq, Soweto, Mbeya. Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa:

Mzee Shirani

Sheikh Muhsin Rashid Mbisa, Imam na Sheikh wa Kata ya Mswiswi

Pamoja na wengine wengi

Wito kwa Waumini

Ujenzi wa nyumba ya Allah ni sadaka endelevu ambayo thawabu zake hazikatiki. Waumini na wahisani wenye nia ya kuchangia ukamilishaji wa msikiti huu wanahimizwa kujitokeza kuunga mkono juhudi hizi.

Allah Barik.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default