Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani Tanga watoa kauli kwamba Tanga ni salama hakutakuwa na maandamano Disemba 9 wawatoa hofu Wananchi wafanye kazi
Na Agnes Mambo Tanga
Viongozi wa Vyama vya Siasa vya upinzani sita mkoa l wa Tanga wamesema wao hawatashiriki maandamano ya nchi nzima yaliyopangwa kufanyika 9 DISEMBA mwaka huu 2025.
Wanasiasa hao wamefanya mkutano wao baina ya waandishi wa habari wa Mkoani humo,lengo ikiwa ni kuihamasisha jamii kulinda amani iliyopo kwa maendeleo endelevu.
Wakizungumza na Waandishi wa habari Hemed Bakari ambae ni Katibu wa Kamati ya amani na uratibu wa vyombo vya siasa Mkoa wa Tanga amesema wamejiandaa kwa namna ambayo ni bora ya kutokuwa na maandamano ili kuepuka madhara yatokanayo na vurugu hizo Kwani asilimia 82 ni vija asilimia zilizobakia ni watu wazima na wazee.
Kiongozi huyo wa Amani mkoa amesema kumekuwa na viashiria vidogo vidogo kwa baadhi ya maeneo zinazoashiria uhamasishaji wa maandamano na kuwatoa hofu wananchi na kuwataka vijana kuacha mihemko ili kuweza kutimiza malengo waliojiwekea
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii Mkoa wa Tanga (CCK) John Mtunguja amesema amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa kuwa karibu na viongozi wa vyama vya siasa ili kuepusha migogoro kwa kufanya mazungumzo ya pamoja.





