MAFUNZO YA COASCO KUIMARISHA UWAJIBIKAJI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA

Xmation Media
By -
0


Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limewajengea uwezo viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika katika uhasibu, ukaguzi wa ndani, TEHAMA na masuala ya kodi, kwa lengo la kuimarisha utawala bora, uwajibikaji, usimamizi wa rasilimali na uendeshaji wa vyama hivyo.

Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu leo, Septemba 23, 2026, katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Alphonce Muro, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapatia washiriki maarifa na zana za kuboresha maamuzi na mifumo ya uendeshaji wa vyama hivyo, huku akisisitiza kuwa thamani ya mafunzo hayo itapimwa kwa mabadiliko yatakayotokea katika Vyama vya Ushirika.

“Tutajua mafunzo haya yameleta tija ikiwa maamuzi ya Bodi yatakuwa bora zaidi, taarifa za fedha zitakuwa sahihi zaidi, sheria za kodi zitazingatiwa kwa wakati, matumizi ya TEHAMA pamoja na udhibiti wa ndani vitakuwa madhubuti zaidi, hoja za ukaguzi zitapungua na wanachama wataona uwazi na uwajibikaji zaidi,” amesema CPA Muro.



Naye, Meneja wa Ilundomatambiko AMCOS zao la Miwa kwa niaba ya Washiriki amesema mafunzo ya COASCO yamekuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa Vyama hivyo

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default