WATU 150,000 KUSHRIKI TAMASHA LA KITAIFA LA UTAMADUNI

Xmation Media
By -
0

 



Na Ashton Balaigwa,MOROGORO

SERIKALI imewataka Wananchi wa Mkoa wa Morogoro waliangalie kwa mapana na kuchangamkia fursa mbalimbali ili kunufaika na kujiongezea kipato  kupitia Tamasha la  Kitaifa la Utamaduni linalofanyika Mkoani humo kuanzia Agosti  25 hadi 29 mwaka huu.


Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Gerson Msigwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye kituo kihistoria cha urithi cha Wapigania uhuru wa Afrika Kusini kilichopo Mazimbu Manispaa ya Morogoro ambapo zaidi ya wageni 150,000 watashiriki .


“ Hapa tulipo ndio mahari ambapo wapigania uhuru wa Afrika kusini walikuwa wakiishi hapa mazimbu,na majengo haya yaliyojengwa kwa mawe na kuna makaburi yao taklibani 97 wakati wa harakati walikaa hapa kwaajili ya mapambano na nchi yetu kama marafiki tulitoa eneo na mengine kama Kongwa ,Dar es Salaam na Kilolo Iringa na leo yamekuwa historia isiyofutika kwakuwa ipo Nyumba aliyokaa Rais mstaafu Nelson Mandela” alisema Msigwa.


Msigwa alisema maandalizi yote ya tamasaha hilo hilo la kitaifa la Utamaduni yamekamilika kwa asilimia 100 na  tayari washiriki wake  wameshawasili siku chache zilizopita,


“ Tayari washiriki wote wameshaingia Morogoro na morogoro imefurika kwa sababu kuna watu wengi wamekuja kwenye tamasha hilo hivyo wakazi wake wakiwemo wafanyabiashara,wauzaji wa vyakula,taasisi mbalimbali zinzotoa huduma za kijamii wachangamkie fursa za kuwepo kwa wageni hao” alisema Msigwa.


Msigwa ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ,alisema Tamasha hilo litafunguliwa rasmi Agosti 26 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Adam Malima,limelenga,kutangaza Utamaduni  na fahari ya nchi ya Tanzania.


Alisema kuwa Tamasha hilo la Kitaifa la Utamaduni lnafanyika kwa kuzunguka mikoa yote nchi na lilianza Dar es Salaa, baadaye Njombe ,Ruvuma na mwaka huu linafanyika Morogoro.


Katibu Mkuu huyo alisema tamasha hilo ni muhimu kwakuwa linaitangaza nchi kitaifa na kimataifa kwakuwa linaleta ustawi wa nchi ya Tanzania .


  Ally  Mkopi ambaye ni msimamizi wa Kituo hicho cha wapigania uhuru wa Afrika ya kusini cha Mazimbu  ,alisema wapigania uhuru hao walifika tangu mwaka 1978 hadi mwaka 1994 walipopata uhuru na kwenda kwao.


Mkopi alisema Rais mstaafu Hayati  Mandela alipotoka gerezani alifikia katika kambi hiyo ya Mazimbu na kulala na kuishi kwa siku kadhaa na mpaka leo ipo kumbukumbu ya nyumba yake alioshi.


“ Kuna historia na tunaitunza mpaka leo ipo nyumba ya Mandela alioishi kwa siku kadhaa na nyumba hiyo pia alikuja kulala aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Mkapa ,kuna makaburi 97 ya wapigania uhuru ambao wengi wao walifariki mwaka 1997” alisema Mkopi.


Mwisho


MAELEZO ya PICHA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Gerson Msigwa,kulia,akimtambulisha msimamizi wa Kituo cha Wapigania uhuru wa Afrika Kusini Ally Mkopi Kwa Waandishi wa Habari wakati alipokuwa akizungumzia tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika mjini Morogoro.

Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default