XMATION DIGITAL YAZINDUA OFISI MPYA; YAHAIDI KUINUA UBUNIFU NA TEKNOLOJIA NCHINI

Xmation Media
By -
0


Na Ashrack Miraji, Dar es Salaam

Kampuni ya Xmation Digital imezindua rasmi ofisi yake mpya katika hafla iliyojaa hamasa iliyowakutanisha waandishi wa habari, wadau wa teknolojia, wageni waalikwa pamoja na wataalamu wa sekta ya ubunifu. Uzinduzi huu umetajwa kuwa hatua muhimu inayoashiria ukuaji na mwelekeo mpya wa kampuni katika kuimarisha matumizi ya teknolojia na ubunifu wa kisasa nchini Tanzania.

Katika hotuba yao, uongozi wa Xmation Digital umeeleza kuwa kusudi kuu la ufunguzi wa ofisi hiyo ni kuandaa mazingira bora na rafiki kwa vijana na wataalamu wanaohitaji kutumia teknolojia katika kutengeneza, kuhariri na kusambaza maudhui yenye ubora wa juu. Wamesema kuwa ofisi mpya ni nguzo muhimu itakayowapa fursa watalaamu wa ndani kubuni kazi zenye viwango vya kimataifa.

Xmation Digital imejikita katika utoaji wa huduma za kidijitali na ubunifu wa kuona, ikiwemo uchapishaji wa majarida, vitabu, mabango, T-shirt zenye nembo, na bidhaa nyingine zinazosaidia taasisi, mashirika na jamii kufikisha ujumbe wao kwa ufanisi na mvuto zaidi. Huduma hizi zimeelezwa kuwa muhimu katika kuhifadhi taarifa, kuimarisha mawasiliano na kujenga utambulisho wa taasisi mbalimbali nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, uongozi wa kampuni hiyo ulisisitiza kuwa dhamira yao ni kuendelea kuwa kitovu cha ubunifu na mawasiliano ya kisasa, huku wakilenga kupanua wigo wa ushirikiano na wadau wanaohitaji huduma bunifu, zenye weledi na zinazoleta matokeo chanya ndani ya jamii. Wameahidi kuboresha zaidi teknolojia wanazotumia ili kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye ubora unaokidhi viwango vya kimataifa.


Katika tukio hilo, shukrani maalum zilitolewa kwa familia, washirika, marafiki na wadau wote walioiongoza kampuni hiyo tangu ianzishwe hadi kufikia hatua ya uzinduzi wa ofisi mpya. Waandishi wa habari pia walipongezwa kwa mchango wao mkubwa katika kusambaza taarifa sahihi na kuiunganisha jamii na dunia ya habari na teknolojia.

Kwa niaba ya timu nzima ya Xmation Digital, uongozi ulihitimisha kwa kusema kuwa uzinduzi huu ni mwanzo wa safari mpya ya ukuaji na mafanikio, wakiahidi kuendelea kushirikiana na vijana, taasisi na jamii katika kujenga mustakabali bora wa teknolojia, ubunifu na uchapishaji nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default