Na Mashaka Mgeta/Agnes Mambo. HANDENI
WAZIRI Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, ameiasa jamii, pamoja na mambo mengine, kuwekeza zaidi kwenye malezi bora kwa watoto.
Mhe. Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo alipomwakilisha Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye ibada ya misa ya Wakfu na kumuweka kitini Kasisi Kanoni Charles Lunda wa Dayosisi ya Handeni mkoani Tanga.
Mhe. Dkt. Mwigulu amesema malezi bora ni jukumu ambalo limekuwa likifanyika vema na kwamba utekelezaji huo unapaswa kuendelezwa.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwigulu amesema Serikali inaendelea kusimamia misingi ya amani, utulivu, umoja na mshikamano nchini, vinadumu.
Naye Askofu Lundu qanaunga mkono hoja hiyo na kusema, haki ya malezi inapaswa kutolewa kwa wavulana na Wasichana
Askofu Lundu amesema, wajibu na sauti za viongozi wa dini katika kutelekeza wajibu wenye maslahi kwa jamii, waendelee kupaza sauti zaidi ipasavyo.
Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Dkt. Maimbo Mndolwa amesema kuanzishwa kwa Dayosisi ya Handeni kunalenga kukabiliana na changamoto zilizojitokezakuliongoza eneo hilo kutokea Korogwe.
Dayosisi ya Handeni 'imemegwa' kutoka sehemu ya Wilaya ya Kilindi na kuchukua eneo lote la utawala wa Serikali katika Wilaya za Handeni na Pangani ambazo awali zilikuwa kwenye Dayosisi ya Tanga.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amemtakia matashi mema Askofu Lundu katika kuiongoza Dayosisi hiyo kwa hekima, busara na upendo kwa watu








