Waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (Mb), amelipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuendelea kujiimarisha katika sekta ya miundombinu wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Jengo la Ramani baina ya Wizara ya Ulinzi na JKT na JWTZ tarehe 03 Agosti 2026 jijini Dodoma.
Dkt. Nyansaho amesema ili JWTZ liendelee kutimiza majukumu yake kwa weledi linapaswa kuendelea kuongeza miundombinu ya kisasa itakayosaidia kukabiliana na matishio ya kiusalama.
Naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ameishukuru Wizara ya Ulinzi na JKT kwa kukamilisha mradi huu muhimu kwa utendaji kazi wa JWTZ.
Hafla ya makabidhiano ya Jengo la Ramani imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Makamanda na Wanadhimu mbalimbali kutoka Wizara ya Ulinzi na JKT pamoja na Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT).

