VETA YABAINISHA UHITAJI WA WA WENYE UJUZI KATIKA FURSA MBALIMBALI NCHINI.

Xmation Media
By -
0

 


NA Deborah Lemmubi-Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi CPA Anthony Kasore amesema kuwa Tanzania inakua kwa kasi katika nyanja mbalimbali ikiwemo miji kupanuka,Viwanda kuongezeka,mirafi ya ujenzi,Utalii na Ukarimu kukua pamoja kilimo kubadilika.

Lakini swali muhimu limekuwa ni nani atafanya kazi hizo kwani zinahitaji kuendeshwa kwa teknolojia mpya,hivyo Wanahitajika Watanzania wenye ujuzi na ndipo umuhimu wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi unapojitokeza kukidhi mahitaji hayo.

CPA Kasore ameyaeleza hayo leo Jijini Dodoma Septemba 4,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari akielezea utekelezaji wa Mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka fedha 2025/26 na mwelekeo wa mwaka 2026/27.



Ambapo amesema ni kweli ajira rasmi zimekuwa na ushindani mkubwa lakini tunapaswa kujiuliza kuwa ni kweli hakuna kazi au kuna kazi ambazo hatuna watu wenye ujuzi wa kuzifanya?


"Tanzania inakua; Uwekezaji unaongezeka; Miji inapanuka; Viwanda vinaongezeka; Miradi ya ujenzi inaendelea; Sekta ya madini inapanuka; Utalii na ukarimu vinaendelea kukua; Kilimo kinabadilika na kuwa cha kisasa zaidi; Nishati inahitaji wataalamu; Usafirishaji na lojistiki vinapanuka na Teknolojia inaingia katika karibu kila eneo la maisha".


"Lakini swali muhimu ni Nani atafanya kazi zote hizi? Nani atajenga? Nani atatengeneza na kuhudumia mitambo? Nani ataendesha teknolojia mpya? Na Nani atahudumia wageni katika hoteli na vituo vya utalii?Jibu ni moja: Tunahitaji Watanzania wenye ujuzi. Na hapa ndipo umuhimu wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi unapojitokeza kwa nguvu kubwa".


"Kuna wakati tunasikia vijana wakisema, “Hakuna ajira.” Ni kweli kwamba ajira rasmi zina ushindani mkubwa. Lakini tunapaswa kujiuliza swali lingine:Je, kweli hakuna kazi, au kuna kazi ambazo hatuna watu wenye ujuzi unaohitajika kuzifanya?Tazama mazingira yanayotuzunguka".


Na kusema kuwa jengo linapojengwa linahitaji fundi wa uashi, seremala, fundi bomba, fundi umeme, fundi wa uungaji na uundaji vyuma, fundi wa mifumo ya viyoyozi na mafundi wengine wengi,Kiwanda kinapojengwa kinahitaji mafundi wa mitambo, umeme, welding, fabrication, instrumentation, automation, maintenance na fani nyingine za kiufundi napo katika Mgodi kunahitaji wenye ujuzi vivyo hivyo.


Na huo ndio wajibu ambao VETA imeubeba kwa uzito mkubwa kuwapa Watanzania, hususan vijana, ujuzi unaowawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi unaokua, kuongeza tija, kupata ajira, kujiajiri, kuunda ajira na hatimaye kuchangia kujenga Tanzania tunayoitaka ifikapo mwaka 2050.


 HIVYO JUKUMU LA VETA NI KUJENGA TAIFA LA WANANCHI WENYE UJUZI.

Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default