Baraza Kuu la Waislam Tanzania ( BAKWATA ) Mkoa Wa Mbeya Leo Limefanya Semina Elekezi Kwa Viongozi Wake Toka Wilaya Zote Sita Za Mkoa Na Uongozi Wa Baraza Mkoa .
Semina Hiyo Ilifunguliwa Na Mkuu Wa Mkoa Mbeya Mh. Jumanne Sagini Abdallah Katika Ukumbi Wa Dkt. Shein Mbeya .
Mkuu Wa Mkoa Mh. Sagini Aliupongeza Uongozi Wa BAKWATA Mkoa Mbeya Chini Ya Sheikh Msafiri Njalambaha Kwa Ubunifu Huo kuwafunza Viongozi Wake .
Mada Tatu Muhimu Ziliwasilishwa Ikiwepo Ijue Katiba Ya Bakwata , Maadili Ya Viongozi Wa Kiislam na Mada Ya Maendeleo .
Washiriki Walifurahia na Kuahidi Kufikisha Elimu Hiyo Wilayani kote hadi Musikitini .
Akiongea kwa Niaba ya Masheikh Wa Wilaya , Sheikh Nurdin Gicha Sheikh Wa Wilaya ya Chunya Alisema Tutaifikisha Elimu Hadi Misikitini .
Akiongea Na Mwandishi Wa Tawfiq Media , Kadhi Wa Mkoa Wa Mbeya Sheikh Mbarazi Ambae Aliwasilisha Mada ya Maadili Ya Viongozi Wa Kiislam alisema huu ni Mwanzo tu , Mazuri zaidi yapo Njiani Inshallah .
Allah Barim
