Kampuni ya Sarga motor (Mahindra) ya Mkoani Simiyu imewataka wakulima kutumia fursa ya mikopo kupata mashine za kuendeshea shughuli za kilimo ili waongeze uzalishaji wa mazao yao.
Meneja wa kampuni hiyo, Alfred Ngenzi amesema leo kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza.
Amesema mikopo yao hutokewa kupitia kwenye mabenki ambapo mkulima hutakiwa kutanguliza asilimia 10 hadi 20 ya thamani ya kitu anachochukua.
"Kutokana na changamoto ya mitaji kwa wakulima mikopo ya zana za kilimo ji ukombozi kwao" alisema Ngenzi.
Bidhaa wanazotoa kwa wakulima ni Trekta horse power 50 hadi 70, power tiller, mashine za kuvuna pamba na mazao mengine, mashine za kulima matuta.
Kwa MAELEZO WASILIANA NAO KWA 0767257028.
