TImu ya Pamba Sports Club imetambulisha kikosi chake kwa msimu huu huku ikiahidi kufanya vizuri katika michezo yake kutokana na kuendelea kupanda juu kwenye ligi hapa nchini.
Mwenyekiti wa Timu ya Pamba Sports Club ambaye pia ni Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Anitha Rwezaula alisema wanapata faraja kuwa wanaendelea kuwa kwenye nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 11 hadi ya saba kwa sasa.
Alisema amefarijika kuona kuwa timu yao inaendelea kusogea mbele kwenye msimamo wa ligi hapa nchini hivyo kuleta matumaini kuwa katika msimu huu mpya watafanya vizuri.
Rwezaula alisema amevutiwa na ujenzi wa uwanja wa Bushirombo kwa kiwangokizuri kinachowezesha hata michezo ya mpira kuchezwa nyakati za usiku.
Alisema anatamani kuwashawishi madiwani wenzake kufika kuona na kuzungumza na halmashaurin hiyo kujua walivyoweza kujenga uwanja kwa kiwango bora.
Katika sherehe hiyo Pamba FC ilipambana na Geita FC ambapo katika mechi hiyo timu mwenyeji katika mtanange huo iliwapiga Pamba FC goli moja.
