MBARAZI ZIARANI MKOANI TABORA, AENDELEA KUPEPERUSHA BENDERA YA UISLAMU

Xmation Media
By -
0

 


TABORA: Sheikh Hassan Mbarazi, Kadhi wa Mkoa wa Mbeya, yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kuendelea kuhamasisha na kuimarisha shughuli za Kiislamu pamoja na kupeperusha bendera ya Uislamu katika maeneo mbalimbali.


Katika ziara hiyo, Sheikh Mbarazi leo amefika Busondo, ambapo alizungumza na Waislamu wa eneo hilo mara baada ya Swala ya Ijumaa.


Akizungumza na waumini hao, Sheikh Mbarazi amesisitiza umuhimu wa Waislamu kushikamana na misingi ya dini, kuimarisha umoja na kuendeleza elimu ya Kiislamu kwa ajili ya kujenga jamii yenye maadili mema.


ATAHADHURIA HADHARA KUBWA PUGA


Kesho, Sheikh Hassan Mbarazi anatarajiwa kushiriki katika hadhara kubwa ya Maulidi ya Mtume Muhammad (S.A.W.) itakayofanyika Puga, mkoani Tabora.


Mbali na kushiriki katika hadhara hiyo, Sheikh Mbarazi anatarajiwa pia kufanya uzinduzi wa Maahadi ya Kiislamu iliyopo Puga, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha upatikanaji wa elimu ya Kiislamu katika jamii.


Baada ya kukamilisha shughuli hizo, Sheikh Mbarazi anatarajiwa kurejea jijini Mbeya siku ya Jumapili, ambapo ataendelea na majukumu yake ya kila siku.


MBARAZI NA UMOJA WA WAISLAMU


Ziara ya Sheikh Mbarazi mkoani Tabora inakuja ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa shughuli zake za kuungana na Waislamu katika maeneo mbalimbali na kuimarisha mshikamano wa Uislamu.


Ikumbukwe kuwa hivi karibuni, Waislamu wa Mbeya walikuwa sehemu ya Umma mkubwa wa Waislamu uliokusanyika jijini Dar es Salaam katika hafla kubwa ya Maulidi ya Nabii Muhammad (S.A.W.).


Katika hadhara hiyo kubwa, Sheikh Hassan Mbarazi aliwakilishwa, huku ujumbe kutoka Mbeya ukiwa sehemu ya tukio hilo lililowakutanisha Waislamu kutoka maeneo mbalimbali.


Allah amuhifadhi Sheikh Hassan Mbarazi na awape wepesi katika majukumu yake ya kuutumikia Umma wa Kiislamu.

Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default