Baadhi ya wananchi waliofika katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) wamefurahishwa na elimu juu ya usimamizi wa shughuli za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asiia.
Wakizungumza katika banda la PURA kwenye tamasha la nne la taifa la Utamaduni linalofanyika viwanja vya Jamhuri Mkoani Morogoro, wananchi hao walikuwa na shauku ya kujua ni lini kama taifa uchimbaji wa mafuta utaanza?
Akijibu hoja hiyo, Mjiolojia kutoka PURA, Lukelo Matimbwi amewaambia wananchi hao kuwa viashiria vya uwepo wa Rasilimali hiyo vipo na tafiti bado zinaendelea, na kwa sasa imegundlika gesi asilia tu.
Tamasha la Nne la Taifa la Utamaduni linatarajiwa kuhitimishwa Agosti 29.


