Na,Agnes Mambo,Tanga.
Watuhumiwa 200 wakamatwa Kwa makosa mbalimbali na wengine 51 wahukumiwa Mkoani Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga Julai 17 kamanda wa polis Almachiusi Mchunguzi Alisema kwa KIPINDI Cha kuanzia Juni 1/2026 hadi Julai 16/2026 Hali ni shwari.
Kamanda Mchunguzi Alisema Jeshi la polisi mkoa wa Tanga limeendelea na uelimishaji kupitia Fassafa ya Polisi Jamii Ili kujenga ushirikiano na Wananchi katika kubaini na kuzuia uharifu.
Alisema sambamba na elimu hiyo pia oparesheni na doria zimefanyika katika maeneo mbalimbali Ili kuwakamata waliofanya uharifu.
Alisema katika KIPINDI hicho,kutokana na oparesheni zilizofanyika Jumla ya watuhumiwa 200 walikamatwa Kwa kutuhumiwa,kujihusisha na uharifu.Uharifu wa aina mbalimbali ikiwemo wa kujihusisha na Dawa za kulevya,Unyanganyi,wizi,kupatikana na mali idhaniwayo kuwa ya wizi nyara za Serikali,uharifu wa miundombinu,noti bandia pamoja na makosa mengine ya jinsi.
Aidha,Watuhumiwa ambao upelelezi ulikamilika walifikiwa Mahakamani na tayari watu 51 wamehukumiwa kifungo,kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo ya kulawiti,kubaka,kuzini na Maharimu,kusafirisha Dawa za kulevya,wizi wa mifugo,kuvunja na kuiba,kujeruhi,kutishia,kuua,kuingia nchini bila kibali pamoja na makosa mengine.
Hata hivyo kamanda Alisema miongoni mwa watuhumiwa kwa makosa makubwa,watuhumiwa wawili walihukumiwa kifungo Cha miaka 30 gerezani Kwa makosa ya kulawiti.
Kamanda Mchunguzi waliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Julis Mustafa ambaye amezini na Maharimu na mwingine ni Kilimo Issaya huku watuhumiwa Mmoja akihukumiwa kifungo Cha miaka 30 gerezani Kwa kosa la kusafirisha Dawa za kulevya ambaye ni Sadiki Waziri.
Alisema watuhumiwa wengine walihukumiwa vifungo vya miaka mitano gerezani Kwa makosa ya wizi wa mifugo na makosa mengine ya Jinsi.
Alisema katika oparesheni dhidi ya Dawa za kulevya watuhumiwa 29 walikamatwa na Dawa za kulevya aina mbalimbali.huku watuhumiwa 14 walikamatwa wakiwa na mirungi bunda 750 yenye uzito wa kilogramu 45 ambapo watuhumiwa 15 walikamatwa na bangi katika mfumo wa misokoto 114,pakiti 126 vifurushi 5 na kete za bangi 120.
Kamanda Mchunguzi Alisema katika oparesheni hiyo Jumla ya Pikipiki 20 zisizo na namba zilikamatwa.
Aidha Watuhumiwa wengine 5 walikamatwa wakiwa na nyara za Serikali na mali zinazohusiana na wanyama pori huku watuhumiwa wengine walikamatwa na vifaa vya miundombinu ya Tanesco,miundombinu ya barabara,noti bandia za fedha za Kenya,televisheni 10,simu za mkononi 25 pamoja na mali mbalimbali zinazodhaniwa kuwa za wizi.
![]() |
| Matukio katika Picha |
Alisema katika kudhibiti ajali za usalama barabarani Kwa KIPINDI hicho Cha Juni mosi hadi Julai 16/ 2026 Jumla ya Madereva elfu 10,028 walikamatwa Kwa kukiuka Sheria za usalama barabarani.
Aliwataja Madereva Kati Yao ni 9 walifugiwa leseni zao za udeleva kutokana na ukiukwaji mkubwa wa Sheria za usalama barabarani ikiwemo Mwendo Kasi
Kamanda Mchunguzi Alisema Jeshi la polisi linaendelea na utoaji wa elimu Kwa wananchi ikiwa ni hatua ya kuendelea kujenga ushirikiano wa kubaini na kuzuia uharifu,oparesheni mbalimbali katika maeneo yote ya mkoa kuhakikisha usalama tunaendelea kuwepo.
Pia kamanda ametoa Wito Kwa wananchi kuendelea kushirikiana na kutoa Taarifa za viashiria na vitendo vya kiharifu Ili kuendelea kudumisha amani na usalama.
Mwisho.







