TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoani Tanga imefanikiwa kuzuia hasara ya Mradi wa sekta ya Elimu shilingi Million 116.2 katika Shule ya Sekondari Chongoleani.
Uokoaji huo wa gharama za ujenzi umetokana na bei za vifaa kuwa chni halisi ya soko na kupeleka mifumo wa manunuzi wa kielekroniki NeST kumkataa zabuni zote kutokana na tofauti ya bei.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga Mkuu wa Takukuru Mkoani Tanga Ramadhani Ndwatah Alisema Takukuru imewezesha Mradi huu kuanza utekelezaji licha ya kuwa fedha hizi zilishatolewa tangu machi 4/2024 .
,,katika ufuatiliaji uliofanywa na Takukuru ilibainika kuwa Kwa upande wa ujenzi wa madarasa,Makadilio ya gharama hususani bei za vifaa vya ujenzi yalikuwa chini ya bei halisi ya soko na kupeleka mifumo wa manunuzi wa Kielekroniki NeST kumkataa zabuni zote kutokana na tofauti ya bei,,Alisema Ndwatah.
Aidha mkuu huyo wa Takukuru mkoa wa Tanga Alisema Kwa upande wa ujenzi wa vyoo,hakukuwa na maandalizi ya Makadilio ya gharama na hivyo taratibu za awali za manunuzi hazikuanzishwa kabisa.
,,Tulichukuwa hatua kuimarisha uwajibikaji na Kwa sasa Mradi huo uko katika Hali nzuri,,Alisema Mkuu wa Takukuru Mkoani Tanga Ndwatah.
Kufanikiwa Kwa kutoka fedha hizo kumetokana na kuwa na ushirikiano mzuri katika kazi zinazofanywa na watendaji wetu wa Takukuru kuwa makini na kufuatilia Kwa ukaribu huduma za miradi ya maendeleo.
Alisema Jumla ya malalamiko 133 yalipokelewa na Kati ya malalamiko 100 asilimia 75.2 yalihusu vitendo vya rushwa.malalamiko ya vitendo vya rushwa yalifunguliwa mijadala ya uchunguzi na mengine yalihamishwa idara ya uchunguzi.
Kamanda mkuu Takukuru Mkoani humo Tanga Alisema Kwa upande wa mashitaka,yamefunguliwa mashauri 11 na Jumla ya mashauri 18 yanaendelea Mahakamani.