Wanawake wapigwa msasa elimu ya mlipa Kodi Tanga.

Xmation Media
By -
0


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga imewapatia elimu ya mlipa kodi na fursa za kibiashara wanawake Wajasiliamali, wafanyabiashara ikiwa ni mkakati wa kuongeza uelewa wa mifumo na sheria za kodi nchini ili kuwajengea mazingira wezeshi yakukuza uchmi wao.

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Castrol John, amesema Mamlaka hiyo inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wanawake katika ukusanyaji wa mapato, akibainisha kuwa kundi hilo sasa limekuwa mstari wa mbele katika uzalendo wa kulipa kodi.

Akizungumza katika Kongamano la Wanawake na TRA mkoani humo amesema  tunatambua mchango wa wanawake kwa sasa wamekuwa kielelezo cha uwajibikaji wa mapato kutoka asilimia 54 hadi 80 katika uzalishaji na uchangiaji wa Kodi hivyo amewaomba kuendelea kuwa namba Moja hapa Mkoani Tanga 

 Naibu Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Ismail Masoud, aliipongeza hatua hiyo na kuwataka watumishi wa TRA kuzidisha kasi ya kutoa elimu kwa walipa kodi ili kuondoa mianya ya sintofahamu inayowakabili wafanyabiashara wengi mkoani Tanga.

“Niwaombe TRA msiishie hapa, endeleeni kutoa elimu kwa wingi ili kukomesha mbinu za ‘janja janja’ za kukwepa kodi Tunataka tushirikiane kikamilifu kufanikisha Dira ya Taifa ya Mwaka 2050 kwa kuwa na mfumo wa kodi wa uwazi na uaminifu,” alisisitiza Masoud.

Masoud alitoa shukrani kwa wadau wa maendeleo, ikiwemo programu ya Good Financial Governance (GFG) na Shirika la GIZ la Ujerumani, kwa ushirikiano wao na TRA katika kuhakikisha elimu ya kodi inafika kwa wanawake na makundi maalum katika jamii.

 Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Wanawake (TWCC) mkoani Tanga Aziza Ramadhan, alisema kongamano hilo limefungua ukurasa mpya kwa wajasiriamali kwani limewapa ujasiri wa kuendesha biashara kwa kufuata taratibu rasmi bila hofu.

“Wanawake wengi walikuwa wakikosa taarifa sahihi, jambo lililosababisha wengi kushindwa kupanua biashara zao kutokana na hofu ya kodi au kutokujua wajibu wao kisheria. Leo tumepata mwanga wa jinsi ya kukua kisheria,” alisema Aziza.

Mjasiriamali na Katibu wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mwajuma Saidi, alibainisha kuwa elimu hiyo imemsaidia kuelewa umuhimu wa kuwa na Namba ya Utambulisho wa mlipa Kodi (TIN) kama kigezo muhimu cha kurasimisha biashara.

WAFANYABIASHARA na wajasiliamali ikiwemo Mwanahabari Agnes Mambo Alisema  elimu hiyo itawasaidia wanawake wengi kubaini kuwa kodi si mzigo wa kuogopesha, bali ni chombo muhimu cha kuimarisha biashara zao na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika uchumi rasmi wa nchini.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default