Muhando Omari Sir Omarry ameongoza Kamati Tendaji ya Chama Mkoa kufanya kikao na Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burhani ofisi kwake ambapo katika kikao hicho Mambo mbalimbali yamejadiliwa katika kuhakikisha Chama kina simama imara.
Lengo la kukutana na mkuu wa mkoa wa Tanga ni kuhakikisha ndani ya Mkoa wa Tanga ni kuweza kuwainua Mafundi kiuchumi kupitia Mikakati Mbalimbali ikiwemo Mafundi wote kuendelea kusajiliwa ndani ya Mfumo wa Chama kwa ajili ya kupata tenda za kazi Kwa urahisi.
Mwenyekiti wa chama hicho amesema katika mazungumzo na mkuu wa mkoa Balozi Dkt Batilda Moja ya mikakati waliyozungumza kuwawezesha kiuchumi,upatikanaji wa tenda za kazi ikiwemo upatikanaji wa Bima ya Afya
Uwekaji wa Akiba za Baadae
Upatikanaji wa Mikopo ya Masharti Nafuu.
Pia wakazungumzia Utatuzi wa Migogoro ya kisheria
Upatikanaji wa kazi kupitia Miradi Mbalimbali ya serikali .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa ameelekeza kuendelea kushirikiana na Viongozi mbalimbali wa Serikalini na Taasisi za Kijamii katika kufikia Malengo ya Pamoja ya Chama ikiwemo uandaji wa Warsha na Makongamano.
Balozi Dkt Batilda aliwataka chama Cha mafundi kuendelea kutoa elimu Juu ya Umuhimu wa Chama Cha Mafundi ili waweze kunufaika kupitia Chama chao.
Mkuu wa mkoa pia alipongeza chama Cha mafundi Kwa hatua walioianza kwamba itakuwa na mafanikio makuwa Kwani kidole kimoja hakivunji chawa.
,,Nitoe pongezi Kwa mafundi wote waliojiunga na chama Cha mafundi kuhakikisha wanakuwa na mawazo ya pamoja katika kuunga mkono juhudi za Serikali kujikwamua kiuchumi Pato la mtu Mmoja Mmoja na kufikia kukuza uchumi wa Taifa kufikia sekta ya ujenzi,,Alisema mkuu wa mkoa wa Tanga Batilda .
,,Natambua chama Cha Mafundi mkoa wa Tanga ni chama imara na muhimu hivyo tunaendelea kushirikiana na kukiunga mkono Ili mafundi muweze kufikia malengo yenu ..alisisitiza Balozi Batilda .
Mkuu wa mkoa Alisema ushirikiano ni muhimu sana katika sekta ya ufundi na ujenzi katika Taifa hili hivyo endeleeni kuwaunganisha mafundi wote na tenda zinapotangazwa tutahakikisha chama tunawashika mkono.
.jpeg)

.jpeg)