Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema wananchi wa Mkoa wa Rukwa wataanza kupata umeme wa gridi kuanzia mwezi mei mwaka huu mara utakapokamilika mradi wa usafirishaji umeme wa msongo wa kV 400 kutokea mkoani Iringa.

Ameyasema hayo katika Mji wa Laela, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba iliyoanza jana mkoani Rukwa.

Hali ya Sasa — Umeme Kutoka Zambia

Ameeleza kuwa, kwa sasa mkoa wa Rukwa unapata umeme kutoka nchini Zambia kupitia mashirikiano ya biashara ya umeme katika nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Power Pool) ambayo yanawezesha nchi wanachama kuuza au kununua umeme pale kunapokuwa na uhitaji ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Ameongeza kuwa, kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha, kazi zinazoendelea ili kuweza kuutumia umeme huo ipasavyo ni ujenzi wa miundombinu imara ya usafirishaji na usambazaji umeme itakayowezesha kufikisha huduma hiyo kwa wananchi wengi.

Mambo Muhimu ya Kujua
Mradi
TAZA — Msongo wa kV 400, Iringa hadi Rukwa
📅
Tarehe Inayolengwa
Mei 2026 (Mwezi wa Tano)
🌍
Chanzo cha Sasa
Zambia kupitia Southern Africa Power Pool (SAPP)
🔥
Lengo la Nishati Safi
80% ya wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo 2034

Nishati Safi ya Kupikia — Lengo la 2034

Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, amesema jitihada mbalimbali zinaendelea ili kuweza kufikia asilimia 80 ya wananchi wanaotumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo 2034 ikiwemo ya kusambaza majiko banifu na mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku.