Na SULEIMAN SHAGATA, MWANZA
WATALAAM wa kutengeneza ngozi katika ubora wa awali, White Cosmetics wa Mtaa wa Rufiji Jijini Mwanza wameongeza huduma zao kuendana na wakati ili kuwezesha ubunifu unaopatikana sehemu nyingine duniani kuwepo katika eneo hili lenye milima maarufu kama Rock City lenye utalii unaopatikana katikakati Jijini hapa.
Wakizindua jana, duka lao la White Cat Cosmetics, Ofisa wa Kampuni hiyo, Samira Mohamed alisema wamekuja na mitindo ya kitaalamu zaidi ikiwa ni pamoja na vifaa , cosmetics za kisasa zaidi kukidhi mahitaji ya muda huu kutoka mataifa ya Korea na Ufaransa ili kuwapatia watanzania huduma ambazo wengine mataifa ya nje hasa yale ya dunia ya kwanza wanapata.
Mashine za kisasa kwa ajili uchunguzi wa ngozi juu ya mahitaji yake zimeletwa, cosmetics zenye ubora zilizo na udhibitisho wa Mamlaka ya Bora Tanzania (TBS) zikiwepo.
"Sisi tunamwangalia mteja ngozi ama nywele za machoni zifanyweje kuwekwa katika ubora mzuri tunafanya kwa kushauriana na mhitaji" alisema Mohamed.
Alisema ngozi huhitaji kurekebishwa kwa watu kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea kwani ndipo ngozi huhitaji marekebisho kuanza kuweza kuwa katika mwonekano nadhifu.
Mohamed alibainisha kuwa wamekuwa wanapokea wahitaji wanaoshiriki sherehe kama harusi zingine zenye kuhitaji mtu kuwa nadhifu wa ngozi na nyusi za macho.
Amesema wanaotumia mitandao ya kijamii ya Instagram , TikTok na Snapchat kutangaza huduma zao wanazotoa ambapo mwenye mahitaji vilevile anaweza kupiga namba hii +255752203805.

