MKUU WA MKOA WA TANGA BALOZI DKT BATILDA BURIAN AOMBA WANANCHI KUCHELEHEKEA KWA AMANI NA UTULIVU KUKARIBIASHA MWAKA MPYA.

Xmation Media
By -
0

Na,Agnes Mambo,Tanga.

MKUU amewaomba Wananchi WA moa wa Tanga kuhakikisha wanasherehekea mwaka mpya 2026 Kwa amani na utulivu.

Akizungumza na Waandishi wa habari amesema sherehe za mwaka huo mpya Mkesha ataungana na Wananchi katika kupokea kwenye viwanja vya uhuru park vilivyopo jijini Tanga.

Alisema Mkesha huo utakuwa wa aina yake Kwa kuwa kutakuwa na wapidhi mbalimbali wakionyesha vyakula vya asili ambavyo vitapingwa na Wananchi watapewa na kula ambapo pia watawashindanisha wapishi na kuapa zawadi.

Aidha, alisema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Ofisi ya Meya wa Jiji la Tanga pamoja na Ofisi ya Mbunge wa Tanga zitawaongoza wananchi kuukaribisha Mwaka Mpya katika Bustani ya Uhuru, ambapo kutakuwa na mashindano ya upishi wa vyakula mbalimbali vya asili ya Tanga, burudani kutoka kwa wasanii tofauti pamoja na chakula cha bure.

Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo amesema mkoa  unaandaa mikakati mbalimbali kuhakikisha unakabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayotarajiwa, ambayo yanaweza kuathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Amesema hayo wakati akitoa ujumbe wake wa Mwaka Mpya kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Burian alisema kuwa taarifa za hali ya hewa zinaonyesha uwepo wa mvua zisizo na uhakika, lakini mkoa tayari umejipanga kwa kuweka mikakati itakayohakikisha unaendelea kuwa na ziada ya mavuno.

Aliwashukuru wakazi wa Tanga kwa mshikamano wao, ushirikiano wa karibu na vyombo vya dola pamoja na msimamo wa amani, ambao uliwezesha mkoa kuepuka hali za machafuko zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo nchini.

Aliwasisitiza wananchi hao kuendeleza msimamo huo kwa manufaa ya ustawi wao na maendeleo ya mkoa kwa ujumla.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default