ORPHAN CARE FOUNDATION YATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUTOA MSAADA

Xmation Media
By -
1


Na Wallace Kapungu


Orphan Care Foundation leo imetembelea kituo cha watoto yatima ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuunga mkono juhudi za malezi na ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.



Katika ziara hiyo, timu ya Foundation ilikabidhi mavazi, nguo, na mahitaji mbalimbali muhimu (basic needs) kwa watoto wa kituo hicho, hatua iliyolenga kuboresha maisha yao ya kila siku.



Mbali na kutoa msaada, wahusika walipata nafasi ya kufurahi, kucheza na kushiriki picha na watoto, ikiwa ni njia ya kujenga ukaribu, upendo na faraja kwao.


Uongozi wa kituo umeishukuru Orphan Care Foundation kwa moyo wa kujitolea, ukisema msaada huo umefika wakati muafaka na utaleta tabasamu kwa watoto waliopo chini ya malezi yao.



Tags:

Post a Comment

1 Comments

Post a Comment
3/related/default