Mwanza: Watoto 55 Wahitimu Chekechea Katika Shule ya Rajendra Ruparell

Xmation Media
By -
0

Na Suleiman Shagata, 

Mwanza Watoto 55 wamehitimu elimu ya awali katika Rajendra Ruparell Pre-Primary School, shule iliyopo katikati ya Jiji la Mwanza, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuanza darasa la kwanza katika shule mbalimbali za kimataifa na za ndani ya nchi. 


 Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Meneja wa shule hiyo Saloni Karia alishukuru ushirikiano mzuri kutoka kwa wazazi, akisema umekuwa mchango mkubwa katika kuhakikisha watoto wanapata mahitaji muhimu ya kielimu na malezi. Karia alisema shule hiyo inapokea watoto kuanzia umri wa miaka miwili, na huwajengea msingi katika maeneo ya utambuzi, tamaduni za makabila yao, michezo, na masomo ya darasani. 


Aliongeza kuwa mfumo wa ufundishaji umejikita katika kuwawezesha watoto kujiamini, kujieleza, kuchora na kucheza — stadi zinazowaandaa kuwa tayari kwa darasa la kwanza. 

 Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Msaidizi Kennedy Dalmas alisema shule inahudumia watoto wa asili tofauti ikiwemo Waafrika, Wahindi na Waarabu, huku ikisisitiza upendo, ushirikiano na kutokuwepo kwa ubaguzi. 


 Dalmas alibainisha kuwa ada ya shule ni TSh 900,000 kwa mwaka, ikiwa inalipwa kwa awamu mbili, na wazazi wanaruhusiwa kufanya majadiliano kuhusu utaratibu wa malipo kulingana na mazingira yao. Shule hiyo inayomilikiwa na familia ya Kihindi iko katika mtaa wa Makoroboi, na inafuata mitaala ya NECTA. Kati ya wahitimu 55, 30 ni wasichana na 25 ni wavulana.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default