MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA NLD ASEMA NITAFUNGUA MASOKO YA NJE KWA WAKULIMA WA MAZAO LUSHOTO.

Xmation Media
By -
0

MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA NLD ASEMA NITAFUNGUA MASOKO YA NJE KWA WAKULIMA WA MAZAO LUSHOTO.

Na,Agnes Mambo,Lushoto, xmation media Tanga

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha NLD, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mhe. Doyo Hassan Doyo, ameendelea na kampeni zake kwa kunadi sera za chama katika eneo la Wakazi,Lukozi, wilayani Lushoto.

Akinadi sera na vipaumbele vyake katika mkutano wa hadhara,uliovuta idadi kubwa ya wafanyabiashara wa mboga mboga, Mhe. Doyo alibainisha changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara hao kuwa ni ukosefu wa masoko ya uhakika.

Alieleza kuwa iwapo biashara hiyo itaandaliwa kwa ubora na ustadi, inaweza kuwanufaisha wananchi na familia zao kiuchumi.

“Mazao haya ya mboga mboga yana soko kubwa la ndani hata nje ya nchi, lakini tatizo ni kwamba hatujaandaliwa mazingira mazuri ya kibiashara.

Kwa sasa mazao yote yanategemea soko moja la Dar es Salaam, na huko nako madalali huwanyonya wakulima.Mkinipa ridhaa, ya kuwa rais wenu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania basi nitahakikisha tunawatafutia masoko ya nje ya nchi ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza thamani ya kilimo chenye tija na manufaa.

Alisema lakini pia,Tutawaleta wanunuzi wakubwa, watasindika mazao yenu na kusafirisha kimataifa Kwa kuwa Jiografia ya Lushoto inaruhusu biashara ya mazao haya kufanyika kwa misimu yote.

Wakati akijinadi Kwa Wananchi wa soko la Lukozi na wafanyabiashara Mhe. Doyo aliikosoa serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kuwa wabunifu katika kuwaendeleza wananchi kiuchumi,hususani WAKULIMA wanaotengemea kilimo Ili kuhudumia familia zao na kubaki masikini.

 Alifafanua kuwa sura ya nne ya Ilani ya Chama cha NLD imebeba ajenda ya kilimo, mifugo, uvuvi na usalama wa chakula, akibainisha kuwa takribani asilimia 70 ya Watanzania hutegemea kilimo kama chanzo kikuu cha kipato.

“Tatizo kubwa ni kuwa kilimo chetu kimeendelea kuwa cha mvua na hakina tija. Hata hivyo, ninyi watu wa Lushoto mnabebwa na jiografia ya eneo hili. Changamoto iliyopo ni upungufu wa miundombinu ya kuhifadhi na kusindika mazao,” alisisitiza.

Aidha, aliwahimiza wananchi wa Lushoto kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu na kumpigia kura yeye, Doyo Hassan Doyo, kwa tiketi ya Chama cha NLD, ili kutimiza adhima ya kubadilisha maisha ya wananchi wa Lushoto na Watanzania kwa ujumla.

Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default