DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AOMBEWA KURA WANANCHI, KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI
Na,Agnes Mambo,xmation media Tanga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdulrahaman amesema amekuja katika mkutano wa hadhara wa wananchi kumuombea kura Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na mgombea, Ubunge,madiwani kwenye uzinduzi wa kampeni Jimbo la Tanga mjini
Aidha katika mkutano huo amewashukuru Wananchi Kwa kuhudhuria mkutano huo Kwa lengo la kusikiliza sera za chama Cha mapinduzi nakuwataka Wananchi wapime hoja za wagombea kisha wafanye maamuzi sahihi ya kuchagua na kupiga kura za ndio Oktoba 29/2025.
Amesema endapo Wananchi mtafanya maamuzi sahihi ya kumchagua rais Dkt Samia Suluhu Hassani na Mbunge,Diwani basi tutahamikisha huduma za Afya zinapatikana Bure hususan magonjwa ya Saratani,Bure na Figo magonjwa atatibiwa Bure.
"Ndugu zangu Wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini tunapata ujasili Kila baada ya miaka mitano tunakuja kusimamia jukwaani kuomba ridha ya kuchaguliwa tena Kwa sababu ya Irani ya miaka mitano tuliahidi na tumetekeleza na bado hatuoni chama kingine kitakachofanya vizuri, hivyo ndio maana tumekuja kuomba Watanzania watupe nafasi nyingine ya kwatumikia ikiwemo wanatanga"Alisema Rajabu.


