MBUNGE LUCY KOMBANI ATEMBELEA SHAMBA DARASA LA AGRIWEZESHA MOROGORO

Xmation Media
By -
0

 



Na Ashton Balaigwa, Morogoro


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Lucy Kombani, ametembelea Shamba Darasa la Taasisi ya Agriwezesha lililopo mkoani humo, kwa lengo la kujifunza na kuona kwa vitendo shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo katika kuwawezesha wakulima.


Akitoa maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo, Mkurugenzi wa Agriwezesha, Deograsia Ignas, amesema taasisi hiyo imeendelea kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo mkoani Morogoro kupitia utoaji wa elimu, ubunifu, matumizi ya teknolojia pamoja na uwezeshaji wa wakulima.



Amesema kupitia programu na elimu mbalimbali zinazotolewa, Agriwezesha imekuwa na mchango mkubwa katika kuwawezesha wakulima kuongeza uelewa na kuboresha shughuli zao za kilimo, huku ikiwafikia wakulima ndani na nje ya Mkoa wa Morogoro.


Kwa upande wake, Mbunge Lucy Kombani amesema amefanya ziara hiyo kama fursa ya kujifunza zaidi kuhusu kazi inayofanywa na Agriwezesha katika kuongeza tija, kuinua kipato cha wakulima na kuifanya sekta ya kilimo kuwa chanzo endelevu cha maendeleo kwa jamii.


Kombani ameitumia pia nafasi hiyo kuipongeza timu nzima ya Agriwezesha kwa kazi wanayoifanya katika kuchochea mabadiliko chanya katika sekta ya kilimo mkoani Morogoro.


Amesema juhudi za kuwawezesha wakulima kupata elimu, kutumia teknolojia na kufanya kilimo kwa tija ni muhimu katika kuimarisha uzalishaji na kuboresha maisha ya wananchi wanaotegemea kilimo.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default