Matumizi ya teknolojia katika kilimo cha pamba ni mhimu katika kuleta mapinduzi ya zao hilo hapa nchini hivyo kufanya wakulima kunufaika na kazi hiyo.
Ushauri huo umetolewa ĺeo jijini Mwanza katika maonesho ya Nanenane kwenye viwanja vya Nyamhongolo na Ofisa Kilimo Kanda ya Magharibi Dotto Ntumba.
Alisema elimu ni mhimu kutolewa kwa wakulima wanaolima zao hilo ili waweze kupata tija ya kilimo chao.
Ntumba alibainisha kuwa kutokana na kuwepo kwa teknolojia ya kunyunyizia dawa shambani kuua wadudu waharibifu mashambani kuanza pamoja na matumizi ya mbolea tofauti kuleta tija sasa elimu ndo mkazo kwao.
Alisema matumizi ya teknolojia kwenye kilimo cha pamba.kitawezesha.kuongeza thamani kwenye mnyororo wa zao hilo ambalo lilijulikana hapo awali kama dhahabu nyeupe.
Naye Ofisa Kilimo Bodi ya Pamba Tanzania Kanda ya Magharibi, Salmath Kisengo alisema wameandaa mashamba darasa yenye kuonesha uasilia wa matumizi ya mbolea mashambani kuwawezesha wakulima kufahamu mbolea zipi huleta mazao mengi.
Alisema uhalisia unaoesha kuwa matumizi ya samadi pekee hayana matokeo ya upatikanaji wa mazao mengi shambani hivyo mbolea hai ndo suluhisho ya upatikanaji mazao mengi.
Aidha Kisongo alisema uzingatiaji wa Kanuni 10 za kilimo cha pamba ni msisitizo unaotakiwa kupewa kipaumbele na wakulima wa mazao ya pamba katika maeneo yao kabla ya kulima na wakati kilimo na uvunaji wa zao hilo.
Msimu wa ununuzi wa pamba nchini unakadiriwa kwa mwaka huu kuwa zaidi ya tani 250,000.

