CHUO KIKUU MZUMBE CHAVUTIA WANAFUNZI NA WADAU WA ELIMU MAONESHO YA MWAHAKO TANGA

Xmation Media
By -
0
CHUO KIKUU MZUMBE CHAVUTIA WANAFUNZI NA WADAU WA ELIMU MAONESHO YA MWAHAKO TANGA

Wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu wametembelea banda la Chuo Kikuu Mzumbe katika Maonesho ya 13 ya Mwahako yanayoendelea jijini Tanga, kwa lengo la kupata taarifa kuhusu fursa mbalimbali za masomo zinazotolewa na chuo hicho.
Waliotembelea banda hilo wameeleza kufurahishwa na ushiriki wa Chuo Kikuu Mzumbe katika maonesho hayo, wakisema kuwa wamepata elimu muhimu kuhusu kozi, udahili na fursa nyingine zinazopatikana chuoni hapo.
Chuo Kikuu Mzumbe, kupitia kampasi yake ya Gombelo iliyopo wilayani Mkinga mkoani Tanga, kinaendelea kutoa huduma za elimu ya juu na kuwafikia wananchi kupitia maonesho na shughuli mbalimbali za kijamii.
📍 Maonesho ya 13 ya Mwahako – Tanga 🎓 Chuo Kikuu Mzumbe – Kampasi ya Gombelo, Mkinga
#MzumbeUniversity #Mwahako2026 #Tanga #Elimu #Mkinga #Gombelo #HigherEducation #Tanzania #XnewsChannel
Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default