CHATANDA: WANANCHI, TUKATAE UVUNJIFU WA AMANI, TUJENGE UCHUMI NA MAENDELEO YETU

Xmation Media
By -
0


NA: MWANDISHI WETU, DODOMA

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, ametoa wito kwa wananchi, kujiepusha na uvunjifu wa amani na badala yake mkazo uwe katika kukuza uchumi na maendeleo.

Chatanda ametoa wito huo, Juni 30, Jijini Dodoma, aambapo amesema wananchi waitumie amani iliyopo katika kufanya shughuli za kujiingizia kipato.

"Katika safari ya maendeleo, amani ni mtaji wa kwanza, amani tuliyonayo tuilinde kwa wivu mkubwa, tuitumie katika kufanya shughuli za maendeleleo kama kilimo, biashara, ufugaji, ujasiriamali, uvuvi, ili nchi yetu izidi kusonga mbele kimaendeleo."

"Tuwakatae wachochezi wa vurugu na machafuko, Tanzania tunafanya vizuri kiuchumi, tuendelee kutunza tunu yetu ya amani ambayo imetusaida kupata maendeleo," amesema Chatanda.

Katika hatua nyingine, Chatanda amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihangaika ndani na nje ya nchi kutafuta fursa za kiuchumi kama biashara na uwekezaji ili kukuza maendeleo.

"Tumtie moyo Rais wetu Dk. Samia, anavyopigania maendeleo inabidi tumuunge mkono, tuwakatae wale wote ambayo furaha yao ni kuona tunamwaga damu wakati wao na familia zao wana uwezo wa kukimbilia nje ya nchi."

"Wanawake na watoto ndiyo wahanga wakubwa pale vurugu zinapotokea, pia tusisahau kuwa vurugu zinaharibu mtiririko mzima wa shughuli za kiuchumi, tuhakikishe tunalinda amani yetu huku tukichapa kazi," ameongeza Chatanda.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default