WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATEMBELEA VIWANDA MKOANI TANGA

Xmation Media
By -
0

 


KUONA SHUGHULI ZA UZALISHAJI NA KUFUFUA VILIVYOKUFA.


Na,Agnes Mambo,Tanga.


WAZIRI wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga amefanya ziara ya kukagua Viwanda na kuona namna vinavyofanyakazi ambapo amebainisha kuweka mkakati wa sera ya Kufufua vilivyokufa.

Alisema hayo wakati wa ziara yake ya siku Moja akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali Mkoani humo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga.



Amesema sera ya Viwanda inafafanua vizuri na kuona vilivyokufa vinafufuliwa na Wananchi wake wanapata fursa za ajira Ili kujikwamua kiuchumi Kwa mtu Mmoja Mmoja na makundi ya vijana kunufaika.

 "Hivi sasa nimetembelea Viwanda mbalimbali nimeona vinafanyakazi 18 hivyo Rai yangu Kwa wananchi wa mkoa wa Tanga wachangamkie fursa na tunaendelea Kufufua vingine Ili kurudisha hadhi ya mji wa Tanga kuwa wa Viwanda"Alisema Kapinga.

WAZIRI Kapinga Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anataka kuona Ile Tanga ya VIWANDA anaiona na Wananchi wake wanapata ajira Ili kujikwamua kiuchumi.

"Sisi Wizara tutahakikisha hivi VIWANDA vya mkoa wa Tanga vinafufuliwa na kurejesha natumaini Kwa wananchi wetu na Mhe.Rais anatamani sana kuona Kila mwananchi Mmoja Mmoja ananyanyuka kiuchumi kupitia hiii sera ya Viwanda inafafanua "Alisema WAZIRI wa VIWANDA na BIASHARA Kapinga.



Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga DKt Batilda Burian amemuomba WAZIRI WA VIWANDA na BIASHARA kuhakikisha Tanga kunajengwa Gati la pili katika Bandari ya Tanga kuongeza uzalishaji Kwani hivi sasa uhitaji upo.

"Mhe.Waziri tukiongeza Gati lingine la pili hakika Tanga uzalishaji utaongezeka mara dufu na mapato yetu yatakuwa Kwa kasi na VIWANDA vyetu bidhaa zao zitaingia sokoni bila usumbufu"Alisema Mkuu wa mkoa wa Tanga.



MKUU wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Alisema hivi sasa Bandari ya Tanga inapokea Meli kubwa za mizigo na kushusha Kwa wakati lakini tuna uhitaji tena wa Gati lingine la pili Ili kuchochea kasi ya ukuwaji wa mapato yetu kimkoa na Taifa Kwa ujumla huku akimshukuru Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassani Kwa kuwekeza fedha nyingi katika bandari ya Tanga na matokeo yake sasa yanaonekana.

Aidha pia Balozi Batilda amesema ufuatiliaji wa VIWANDA mara Kwa mara umeanza kuzaa matunda na Leo tunashuhudia kuona VIWANDA vilivyokufa vinafufuliwa na tumetembelea kujionea wenyewe hivyo tunashukuru Wizara pamoja na mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassani.



Amesema sisi kama mkoa tutahakikisha Kila Wilaya inakuwa na VIWANDA na vile vya zamani vinafufuliwa Kwani baadhi ya Viwanda vilikuwa kwenye majaribio na hivi sasa tayari vimekwisha kuanza kazi.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default