Mamy Cakes Kuja Kivutio Maonesho ya Keki Msimu wa Krismasi Mwanza

Xmation Media
By -
0


Na Suleiman Shagata – Mwanza


Kampuni ya Mamy Cakes, iliyopo Mtaa wa Lumumba katikati ya Jiji la Mwanza, mkabala na Supermarket ya Little More barabara ya U-Turn, imetangaza kushiriki kwa mara nyingine tena katika maonesho maalum ya keki msimu wa Krismasi (X-Mass) yanayotarajiwa kuanza tarehe 20 hadi 26 mwezi huu.


Maonesho hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Ghandhi Hall uliopo Kemondo, yakilenga kuwapatia wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani fursa ya kufurahia bidhaa bora za mikate, keki na vinywaji vilivyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.


Huduma Bora na Bidhaa Zenye Ubora wa Hali ya Juu


Akizungumza leo Jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Mamy Cakes, Mariam Hassan, alisema kampuni hiyo imejipanga kuwahudumia wateja kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia ladha, usafi na mahitaji ya kila mteja.



> “Tunatarajia kuwapatia wakazi wa Mwanza na viunga vyake aina bora za keki pamoja na vyakula vingine vilivyotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, sambamba na huduma ya kuwafikishia wateja bidhaa waliko,” alisema Hassan.




Aliongeza kuwa Mamy Cakes pia ina huduma ya keki za kunywea chai, ambapo mteja anaweza kuagiza na kufikishiwa popote alipo, pamoja na keki za sherehe mbalimbali ikiwemo harusi, birthday, send-off na hafla za kijamii.


Aina Mbalimbali za Vyakula na Vinywaji


Mkurugenzi huyo alitaja baadhi ya bidhaa zitakazopatikana katika banda lao wakati wa maonesho kuwa ni pamoja na:


Ice cream


Coffee na Cappuccino


Cookies


Chai cakes


Cup cakes


Pop corn


Milk cakes (chocolate & coffee)


Milk shakes (chai masala na ladha nyingine)



Keki kwa Viwango na Mahitaji ya Wateja


Hassan alisema keki wanazotengeneza hupatikana kwa viwango tofauti kulingana na mahitaji ya mteja, jambo linalowawezesha watu wa makundi mbalimbali kumudu huduma zao.


Alisema lengo la Mamy Cakes katika maonesho ya mwaka huu ya msimu wa Krismasi ni kuwapa wateja huduma bora itakayojenga imani, na kuwafanya waendelee kuitumia kampuni hiyo katika matukio yao ya kijamii na sherehe mbalimbali.



Ubora wa Malighafi Ndio Siri ya Ladha


Akizungumzia ubora wa bidhaa zao, Hassan alisema Mamy Cakes hutumia malighafi bora ikiwemo maziwa, vanilla, chocolate, pamoja na siagi za viwango vya juu kama Blue Band, Prestige, KCC, Kerrygold na nyinginezo.


Kwa maandalizi hayo, Mamy Cakes inaahidi kuwa kivutio kikubwa katika maonesho ya keki msimu wa X-Mass, na kuwakaribisha wakazi wote wa Mwanza kufika Ghandhi Hall Kemondo kuanzia tarehe 20 hadi 26 mwezi huu.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default