Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo alipowasili katika eneo la Itega jijini Dodoma kwa ajili ya kuhani msiba nyumbani kwa marehemu Jenista Mhagama. Amesema marehemu Mhagama alikuwa kiongozi makini na mchapakazi, aliyejitoa kwa dhati katika kutumikia Jimbo la Peramiho, Chama Cha Mapinduzi (CCM), na maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
“Mama Jenista alikuwa kiongozi aliyekuwa na uzalendo na moyo wa kuitumikia nchi bila kuchoka. Taifa limepata pengo kubwa sana kutokana na kuondoka kwake,” amesema Makamu wa Rais.
Aidha, Makamu wa Rais ameifariji familia ya marehemu pamoja na waombolezaji wote, akiwataka kuwa na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu, huku akiwaombea watoto na ndugu wa karibu wawe na ujasiri wa kukubali msiba huo kama sehemu ya safari ya maisha ambayo wanadamu wote hupitia.
“Tunawaombea faraja na nguvu katika kipindi hiki. Kuondoka kwake ni mapenzi ya Mungu, na ni njia ya mwanadamu wote,” amesema.
Marehemu Jenista Mhagama atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika siasa, uongozi, na usimamizi wa shughuli za maendeleo nchini.
.png)

.jpeg)