WAFURAHIA KUKARIBIA KUMALIZIKA KWA UJENZI WA DARAJA - MWANZA

Xmation Media
By -
0

 Na SULEIMAN SHAGATA MWANZA 

WAKAAZI wa Mtaa wa Mabatini Jijini Mwanza wameelezea furaha yao kufuatia kukaribia kukamilika kwa ujenzi wa daraja na barabara kupitia Kampuni ya Kizalendo ya Nyanza Road Works Ltd kutatua changamoto ya mafuriko kipindi cha masika katika eneo hilo.

Wakizungumza Leo kwa nyakati tofauti walisema awali walikuwa wakikumbwa na adha ya kujaa kwa maji kutokana na kuzibwa taka kwenye matundu ya daraja hilo kwani lilikuwa dogo hivyo kusababisha mafuriko.



Mwenyeki wa Mtaa wa Mabatini Kaskazini Hamis Nassoro kukamilika mradi huo itakuwa ufumbuzi wa magari yanayoingia Jijini Mwanza na yanayotoka katika vipindi vya mvua kwani kulikuwepo changamoto ya mafuriko kwenye mto Milongo.

Alisema mafuriko yaliyokuwa yakitokea yalisababisha madhara kwa watu na mali zao hivyo umahiri mkandarasi mzalendo Nyanza Road Works unaleta suluhu ya changamoto hiyo kwa sasa.

Naye mkazi wa eneo hilo Haji Katimba alipongeza kampuni hiyo kwa kutoa ajira ya ujenzi wa daraja hilo kwa wazawa wa mtaa huo.

Katimba alipongeza kampuni hiyo ya Kizalendo ya Nyanza Road Works kwa kushirikiana na Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kwa kuwa na utamaduni wa kukaa kwa pamoja na wananchi katika mtaa huo kujadiliana nao juu ya ujenzi wa mradi huo.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default