KIJANA MWENYE SELIMUNDU MWANZA AOMBA MSAADA WA BAJAJI KWA RAIS SAMIA

Xmation Media
By -
0

Na SULEIMAN SHAGATA, MWANZA

Kijana anayesumbuliwa na maradhi ya selimundu jijini Mwanza amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kumsaidia bajaji ili aweze kujipatia kipato kutokana na adha anayoipata ya kuuza koni hasa nyakati za masika.

Akizungumza leo jijini hapa, Masoud Shabani (39), mkazi wa Mkuyuni, alisema wazazi wake wote walifariki akiwa bado mdogo na hawakuacha nyumba, hivyo fedha anazopata amekuwa akizitumia kununulia dawa na kulipia chumba anachoishi.



Vile vile, Shabani alisema anaomba pia msaada kwa viongozi wengine akiwemo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi, Said Bakheresa, pamoja na mtu yeyote atakayeguswa na hali yake.

Hivi karibuni, kufuatia mvua iliyonyesha kwa zaidi ya saa sita jijini Mwanza, nyumba aliyokuwa anaishi ambayo alipewa tu kwa huruma iliweza kuharibika vibaya kutokana na upepo, na kwa sasa hana mahali pa kuishi.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default