Simba Day 2025 Yatingisha Dar, Simba SC Waikaribisha Gor Mahia
Na Iyan Juma, Xmation Media
Dar es Salaam, Septemba 10, 2025 – Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam uligeuka kitovu cha burudani, michezo na mshangilio usio na kifani baada ya maelfu ya mashabiki kujitokeza kushuhudia kilele cha Simba Day 2025.
Tamasha hili, ambalo hufanyika kila mwaka kuashiria mwanzo wa msimu mpya wa soka, liliambatana na shamrashamra za kipekee zikiwemo burudani za muziki, utambulisho wa kikosi kipya cha Simba SC na mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Uwanja Umefurika
Kwa mara nyingine tena, mashabiki wa Simba walionyesha nguvu na mshikamano wao kwa kujitokeza kwa wingi. Tiketi zote ziliuzwa mapema, na zaidi ya mashabiki 60,000 walijaza uwanja, wakiashiria hamasa kubwa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
---
Burudani ya Kipekee
Mbali na soka, jukwaa la burudani lilichangamka kupitia wasanii wakubwa wa muziki nchini akiwemo Mbosso, Chino Kidd na Joh Makini, waliotoa shoo zilizozidisha hamasa ya mashabiki.
Msanii Mbosso, ambaye ni nyota wa Bongo Fleva kutoka WCB Wasafi, aliingia Uwanja wa Mkapa kwa uingiaji wa kipekee sanaa uliowasha shangwe kubwa. Mashabiki walilipuka kwa furaha na kuimba naye kwa sauti moja, jambo lililoongeza ladha ya tamasha na kuufanya usiku huo kuwa wa kukumbukwa.
---
Kikosi Kipya Chawashangaza Mashabiki
Uongozi wa Simba SC pia ulitumia siku hiyo kutambulisha rasmi wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu wa 2025/2026. Hatua hiyo ilipokelewa kwa heshima kubwa na mashabiki waliokuwa na shauku ya kuona nyota hao wapya wakiongeza nguvu ndani ya kikosi.
---
Mechi ya Kirafiki: Simba SC vs Gor Mahia
Mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia uliweka ukomo wa shamrashamra, huku ukionekana kama kipimo cha kiwango cha Simba kuelekea msimu mpya. Licha ya kuwa mechi ya kirafiki, mashabiki walishuhudia ushindani mkubwa uliodhihirisha ukubwa wa timu hizi mbili za Afrika Mashariki.
---
Ujumbe kwa Mashabiki
Kwa mashabiki wa Simba, Simba Day si tukio la kawaida. Ni zaidi ya mchezo wa mpira – ni siku ya kuonyesha mshikamano, kusherehekea historia ya klabu na kuashiria mwanzo wa safari mpya ya mafanikio.







.jpg)
