Na Neema
Geita, Tanzania
Paschal, ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Udiwani katika Kata ya Butobela, ni miongoni mwa wadau waliotoa mchango mkubwa katika juhudi za kuinua sekta ya wachimbaji wadogo kupitia uwekezaji, ushirikiano na ubunifu katika shughuli za uchimbaji.
Akizungumza katika tukio hilo, wadau mbalimbali walimpongeza King Mapungo kwa moyo wake wa kujitolea na kujihusisha moja kwa moja na shughuli za wachimbaji wadogo, hatua ambayo imeleta mabadiliko chanya katika jamii ya wachimbaji mkoani Geita.
“Paschal ni mfano mzuri wa kiongozi kijana mwenye maono. Ameonyesha dhamira ya kweli ya kusaidia wachimbaji wadogo kupiga hatua kimaendeleo,” alisema mmoja wa viongozi wa chama cha wachimbaji.
Tukio hilo limekusanya wadau kutoka sekta binafsi, viongozi wa serikali, wachimbaji wadogo, pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali, likiwa na lengo la kutambua na kuhamasisha ushiriki wa wadau katika maendeleo ya sekta ya madini.
Kwa muda mrefu, Paschal Mapungo amekuwa nguzo muhimu katika kuhamasisha vijana kushiriki katika sekta ya madini kwa njia endelevu, huku akichangia ajira na ukuaji wa kiuchumi katika eneo la Butobela na maeneo jirani.


