Bahati Kenneth Ndingo Kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbarali
Mwandishi Xmation Media - Ashrack Miraj
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua rasmi Mheshimiwa Bahati Kenneth Ndingo kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Mbarali kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa.
Uteuzi huo umetangazwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla, tarehe 23 Agosti 2025, wakati akitoa taarifa ya maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
