![]() |
| Agnes Mambo org-image 01 |
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga (TangaUWASA) imesema mradi wa Hatifungani ya Kijani umelenga kusambaza maji na kutatua changamoto kwa wananchi wa Wilaya ya MUHEZA,Mkinga,Pangani naTanga ifikapo 2026.
Akizungumzia kukamilika Kwa miradi huo mkubwa Mkurugenzi wa usambazaji maji Mhandis Salum Ngumbi amesema unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2026, ambapo mradi huu utawezesha wananchi kupata huduma ya majisafi na salama kwa masaa 24 .
Aidha,Mkurugenzi wa Usambazaji Maji, Mhandisi Salum Ngumbi, wakati wa ziara ya Waandishi wa habari mkoa wa Tanga ya kutembelea na kujionea hatua mbalimbali za maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Hatifungani pamoja na kupata taarifa ya hali ya huduma amesema mradi huu unathamani ya shilingi billion 53.12.
Mhandisi Ngumbi aliwaeleza wanahabari wakiwa katika mradi huo kuwa umelenga kuongeza kiwango cha uzalishaji na usambazaji wa maji kutoka mita za ujazo 45,000 hadi mita za ujazo 60,000.
Pia Mhandisi Ngumbi amesema kupitia uboreshaji w4a miundombinu ya usambazaji maji kwa kulaza mabomba makubwa yenye kipenyo cha mm 600 kwa urefu wa kilomita 6.4 kutoka kituo cha kusukuma maji Mabayani hadi katika Mtambo wa kuzalisha maji wa Mowe, Upanuzi wa kituo cha kusafisha maji na kutibu maji cha Mowe, Ujenzi wa tangi la kuhifadhia maji lenye ukubwa wa mita za ujazo 35,000.
Mhandisi Ngumbi,Alitaja mahitaji mengine,Kuongeza mtandao wa usambazaji maji mwa maeneo ya pembezoni, ukarabati wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka, Kufunga dira 10,000 za malipo kabla sambamba na kuimarisha shughuli za utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TangaUWASA, Dkt. Fungo Ali Fungo amewashukuru waandishi wa habari wa Tanga kwa ushirikiano mzuri wanaounoesha kwa Taasisi ambapo amesema kuwa katika mwaka huu Mamlaka imeendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa lengo la kuendelea kuimarisha na kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.
Ziara hiyo imelenga kuwawezesha waandishi wa habari wa Tanga kutembelea na kujionea maendeleo ya utekelezaji mradi wa Hatifungani ambapo walitembelea Bwawa la kuhifadhia maji la Mabayani na Mtambo wa kutibu na kuzalisha maji wa Mowe ambapo mradi unatekelzwa.
Hivi sasa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira inatekelezwa Kwa asilimia 88 na kukamilika Kwa mradi huo itafikia asilimia 100 katika maeneo yote yaliyofikiwa na mradi wa hati fungani ya kijani.
Naye afisa uhusiano wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga (Uwassa) Devota Mayala amesema tanki la maji litakuwa la pili Tanzania Kwa ukubwa MITA za ujazo 35,000 ukitoka la mkoa wa Hinyanga kuwa la kwanza lenye MITA za ujazo 37,000.
Mayala ameomba ushirikiano Kwa waandishi uelendlee Ili kuleta tija na maendeleo Kwa Wananchi na jamii Kwa ujumla.
.png)
.png)



