MELI KUBWA YA MZIGO KUTOKA IRAN YATIA NANGA BANDARI YA TANGA.

Xmation Media
By -
0

 


Na,Agnes Mambo,Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga amesema wataendelea kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na nchi ya Irani Kwa kufanyabiasha ikiwemo kubadilishana bidhaa Kwa bei nafuu Kwa kuanzisha VIWANDA vidogo vidogo vya machine za uzalishaji bidhaa mbalimbali.



Aidha Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya sita Kwa maboresho ya Bandari ya Tanga yameendelea kuzaa matunda kutokana na kupokea Meli kubwa za mizigo mara kwa mara na mapato ya kiuchumi kuongezeka mara dufu.

Pongezi hizo amezitoa Novemba 28 akiwa katika Bandari ya Tanga baada kupokea Meli kubwa ya mizigo yenye tani elfu 13 kutoka nchini Irani iliyobeba makontena 463 kati ya hayo makontena 261 mizigo ya ndani na makontena 182 ambayo yanasafirishwa kwenda nchi za Afika Mashariki.



Akizungumza na wadau mbalimbali ikiwemo wafanya biashara,wadogo wamashiga na wakati katika bandari ya Tanga mara baada ya kupokea Meli kubwa ya Moja Kwa Moja kutoka nchini Iran alitoa pongezi hizo huku akisisitiza suala la amani limeleta mafanikio.

Dkt Batilda alieleza maajenti wa Meli hiyo kwamba ni vyema kushirikiana Kwa ukaribu katika kubadilishana bidhaa kwenye masoko Ili kupanua WiGo wa mnyororo wa thamani na kuongeza ajira za kibiashara na ushindani kwa vijana wa Tanga na Irani.

"Hapa Mkoani Tanga tuna MAZAO ya BIASHARA ambayo wenzetu hawana kama viungo vya chai,zao la Korosho,Mkonge,Madini ya Dhahabu ya Glafeiti,Vito,hivyo tunaweza tubadilishana na kutengeneza mtandao vijana kujiajili wenyewe hata wale waliomaliza vyuo ambao bado hawajapata ajira"Alisema Dkt Batilda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanga Adadi Kolimba ameishukuru Serikali Kwa kuboresha bandari ya Tanga Kwani hivi sasa uchumi katika Halmashauri ya Jiji la Tanga umeimarika kutokana na kupata meli nyingi za mizigo.



Kolimba amesema wanatengemea kuona wafanyabiashara na wasafirishaji wa mizigo,madereva kuanza kupata kazi na tenda kufuatia bandari yetu kuimarika na kupokea Meli kubwa za mizigo ya uhakika.

"Wafanyabiashara wa Tanga mnaoshuhudia Meli hii kubwa kutoka nchini Iran fanyeni bidii kubadilishana mizigo na masiliano na nchi hii Ili kujenga uchumi wa pamoja Kwani sisi Serikali tupo na lengo letu nikuwaunganisha Ili kuweza kujikwamua kiuchumi badala ya kusubiri ajira mnaweza kujiajili wenyewe"Alisema DcTanga Kolimba.

Pia ameishukru Serikali wakati alipofika Bandarini kupokea Meli kubwa ya mizigo wa makontena 463 kutoka nchi Irani ambayo ilitumia siku nane hadi kufikia Novemba 27 katika bandari ya Tanga.

Kwa upande wake kaimu Meneja wa Bandari,Peter Milanzi amesema Kwa mara ya kwanza Bandari ya Tanga kuandika historia ya kupokea Meli kubwa ya Moja Kwa Moja kutoka nchini Irani iliyofahamika Kwa Jina la Uleni Kontena MV Pania.



Amesema tunayofuraha kubwa kutokana kwamba tumezoea kupokea Meli ndogo lakini hivi sasa tunapokea Meli kubwa hivyo tunashukuru rais Dkt Samia Kwa kuwekeza fedha nyingi kuboresha Bandari ya Tanga na kuandika histori ya kuongezeka Kwa mapato.


Amesema Meli hii imechukuwa siku nane kutoka Irani kuja Tanga Moja Kwa Moja.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default