Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amezindua rasmi Kozi ya Maabara kwa ngazi ya Stashahada

Xmation Media
By -
0


Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR )

Tarehe 06.12.2025katika kilele cha Mahafali ya 13 ya Zanzibar School of Health (ZSH), hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Maozedong, Wilaya ya Mjini Unguja.

Uzinduzi huo ulioashiriwa kwa kukata utepe, umeelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha rasilimali watu kwenye sekta ya afya visiwani Zanzibar, hususan katika eneo la uchunguzi wa maabara ambalo limeendelea kuhitajika zaidi kutokana na changamoto za afya za sasa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Hemed ameupongeza uongozi wa Zanzibar School of Health kwa kuendelea kuwekeza katika elimu ya afya na kuongeza kozi zinazokidhi mahitaji ya soko la kazi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa vijana kujikita katika taaluma za afya ili kuongeza wataalamu watakaosaidia kupunguza mzigo katika hospitali na vituo vya afya.

Kwa upande wao, viongozi na wakufunzi wa ZSH wamesema kuwa kozi hii mpya ya Maabara inalenga kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa kisasa, uwezo wa kufanya uchunguzi wa kitabibu, na kuendana na mabadiliko ya teknolojia ya afya duniani.

Mahafali hayo yameshuhudia wahitimu kutoka kada mbalimbali za afya wakitunukiwa vyeti na stashahada, ikiwa ni pamoja na uuguzi, famasia, huduma za dharura na sasa Maabara, ambayo imekuwa kozi mpya kuanzia mwaka huu.

Uzinduzi huu umeonekana kuwa ongeza thamani kubwa katika mkakati wa Zanzibar wa kuboresha huduma za afya kupitia mafunzo ya kitaalamu na uongezaji wa kada za afya zinazohitajika kwa kiwango kikubwa.



Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default