Diwani wa Kata ya Nyamagana Atoa Wito wa Kudumisha Amani Kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka

Xmation Media
By -
0


Neema : Xnews  Mwanza Tanzania 

Diwani wa Kata ya Nyamagana kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Frank Chacha, amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hususan kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.


Akizungumza leo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara inayotekelezwa chini ya mpango wa maendeleo wa IRANI 2025/2030, Dkt. Chacha alisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo na ni tunu muhimu kwa Taifa.



> “Amani ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli. Nawahimiza wananchi wa Nyamagana kuilinda na kuidumisha amani, hasa kipindi hiki cha sikukuu ambapo mikusanyiko huwa mingi,” alisema Dkt. Chacha.

Katika ziara hiyo, Diwani huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa ngazi ya kata, ambapo walitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa mita 350, uliopo Mtaa wa Idara ya Maji – Capri Point, chini ya usimamizi wa Ofisi ya ODC Nyamagana.



Dkt. Chacha alieleza kuridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi huo, akibainisha kuwa barabara hiyo itarahisisha usafiri, kuinua shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wakazi wa eneo hilo.


Aidha, aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na viongozi wao katika kulinda na kusimamia miradi ya maendeleo, ili iweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii.



Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za uongozi wa kata ya Nyamagana kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ubora na kwa kuzingatia mahitaji ha

lisi ya wananchi.







Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default